Tag Archives: upcoming

Gospel vibes

Karanja Kimani

Susan: Susan nimwimbaji ambaye anapiga nyimbo za injili, ambapo natoka katika eneo la western.

Karanja: una albums ngapi?

Susan: kwa sasa nikona albums mbili na kuna wimbo mmoja ambao ni single song, nimeutoa.

Karanja: mipango yako kama mwimbaji wa nyimbo za injili ni ipi?

Susan: mipango yangu, ninataka niimbe na nipenye Zaidi siokwamba niwezekusikika hapa Kenya tu, bali katika maeneo mbalimbali nchi zanje, na wakati ninapoimba nataka hizo nyimbo ziwe za kumkuza mtu, ziweze kumfanya mtu yaani kama ulikuwa mnyonge, unakuwa unasikia unafarijika ndani ya moyo wako, ziwe nyimbo za kuguza.

Karanja: neno ungependa kuwaambia wanamuziki wanaochipuka.

Susan: jambo la kwanza ambalo ningetaka kuwaambia waimbaji ambao ndio wanaipuka ama matamanio yao ni kuwa wanataka wakaweze kumtukuza Mungu katika nchi za injili, jambo la kwanza, kunachangamoto, utavumilia wakati ambapo umestep mguu wako kwenye hatuahiyo, cha kwanza utavumilia challenges majaribio ni mengi, utakapo ona mwingine jambo limemtendekea, usivunjike moyo, nenda kwa magoti, mwombe Mungu mwambie Mungu, mimi katika hii safari nahitaji mimi pia nikaweze kukutukuza katika hizi nyimbo lakini haya majaribu naomba Mungu ukaweze kuniwezesha na Mungu atakuwezesha.